Friday, December 12, 2025
spot_img
HomeMichezoShabalala awaita mashabiki Yanga Mkapa

Shabalala awaita mashabiki Yanga Mkapa

Beki mpya wa Yanga, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi Ijumaa ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa kumpokea rasmi kwenye kilele cha Wiki ya Mwananchi.

Amesema anashukuru mapokezi aliyoyapata na ameahidi kupambana kuhakikisha Yanga inatetea mataji yake na kushinda mengine.

Tshabalala, aliyejiunga na Yanga akitokea Simba baada ya kuitumikia kwa miaka 11, atatambulishwa rasmi siku hiyo ambapo Yanga itacheza na Bandari FC ya Kenya.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Ali Kamwe, amesema usajili wa Tshabalala ni mkubwa na umewaacha wapinzani na pengo gumu kuziba.

Aidha, Kamwe ametangaza kuwa siku hiyo kutatangazwa wachezaji wapya, kutakuwa na burudani na mechi za utangulizi, huku wachezaji wa zamani pia wakitambulishwa.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments