Thursday, December 18, 2025
spot_img
HomeAfyaKilimanjaro: Wito wa utafiti kuhusu watoto kuzaliwa na magonjwa ya moyo

Kilimanjaro: Wito wa utafiti kuhusu watoto kuzaliwa na magonjwa ya moyo

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, ameishauri Hospitali ya Rufani ya Kanda ya KCMC kufanya utafiti wa kina kubaini sababu ya ongezeko la watoto kuzaliwa na magonjwa ya moyo.

Alitoa wito huo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya siku 90 za kuchangia fedha kumalizia jengo la matibabu na upasuaji wa moyo katika hospitali hiyo.

Kwa upande wake, Prof. Kajiru Kilonzo, Mkuu wa Idara ya Tiba KCMC, alisema magonjwa yasiyoambukiza (NCDs) yanaongezeka kwa kasi Kanda ya Kaskazini, huku magonjwa ya moyo yakiongoza kwa vifo.

Naye, Dk. Ronald Mbwasi, Mkuu wa Idara ya Moyo kwa Watoto, alieleza kuwa kati ya watoto 1,000 wanaozaliwa hai, 17 hukumbwa na matatizo ya moyo, na takribani watoto 4,000 huzaliwa kila mwaka na changamoto hizo katika kanda hiyo. Hata hivyo, wengi hutambulika wakiwa wamechelewa.

Aidha, Mkurugenzi wa Tanlink Health Care Foundation, Dk. Siraj Mtulia, alisema Tanzania inapeleka wagonjwa zaidi ya 2,000 nje ya nchi kila mwaka kwa matibabu ya moyo, jambo linalogharimu taifa zaidi ya Shilingi bilioni 20.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments