Tuesday, December 16, 2025
spot_img
HomeMichezoSimba yaelekea Botswana Mechi ya Ligi ya Mabingwa

Simba yaelekea Botswana Mechi ya Ligi ya Mabingwa

Kikosi cha Simba SC kimeanza safari kuelekea nchini Botswana kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United, unaotarajiwa kupigwa Septemba 20 kwenye Uwanja wa Obed Itani Chilume.

Hii itakuwa ni hatua muhimu kwa Simba kwani mchezo huo ni wa kwanza kwao kwenye mashindano ya msimu huu ya CAF Champions League, wakihitaji kuanza vyema ili kujipa nafasi ya kusonga mbele hatua zinazofuata.

Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa bado na kumbukumbu ya kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga SC kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa jana. Hata hivyo, viongozi na benchi la ufundi wamesisitiza kuwa kikosi kipo tayari kurekebisha makosa na kuonesha ubora wao kimataifa.

Meneja wa timu ameeleza kuwa safari ya Botswana ni mwanzo wa kampeni mpya za Simba barani Afrika, na wachezaji wapo kwenye morali kubwa kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ugenini kabla ya mchezo wa marudiano jijini Dar es Salaam.

Wapenzi na mashabiki wa Simba pia wametakiwa kuendelea kuipa sapoti timu yao, wakiamini kuwa msimu huu Wekundu wa Msimbazi wana nafasi kubwa ya kurejea kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa na kwenda mbali zaidi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments