Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema mshikamano uliopo kati ya Tanzania Bara na Zanzibar umeiheshimisha Tanzania ulimwenguni.
Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo, Alhamisi Septemba 18, 2025, alipozungumza na wananchi wa Nungwi visiwani Zanzibar, katika mkutano wake wa kampeni za urais.
Amesema pande zote mbili za muungano zimefanya kazi kwa pamoja kukuza uhusiano wa kidiplomasia na hivyo jina la Tanzania limekua ulimwenguni.
“Heshima tunayoipata ulimwenguni, ni kwa sababu ya umoja na mshikamano wetu kama Tanzania na kukuza jina letu,” amesema.




