Monday, December 8, 2025
spot_img
HomeHabariDkt. Samia: Tanga kuwa bohari ya mafuta, gesi

Dkt. Samia: Tanga kuwa bohari ya mafuta, gesi

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema mkakati wa Serikali yake katika miaka mitano ijayo ni kuufanya Mkoa wa Tanga kuwa bohari ya mafuta na gesi.

Hatua hiyo, amesema itafikiwa kupitia uboreshaji wa Bandari ya Tanga, itakayohifadhi na kupokea nishati hiyo, kama ilivyoamriwa na Serikali yake.

Dkt Samia ameyasema hayo, leo, Jumatatu Septemba 29, 2025 alipozungumza na wananchi wa Tanga Mjini, wakati wa mkutano wake wa kampeni za urais, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi.

“Bandari ya Tanga, inakwenda na maamuzi tuliyoyafanya ya kuwa Tanga ni bohari ya mafuta na gesi. Na hilo, litachangia kuzalisha ajira mpya nyingine 2,100 ndani ya Tanga. Hili linakwenda kunyanyua uchumi wa Wana Tanga,” amesema.

Mradi wa Bandari ya Tanga, amesema unafungamana na mradi wa Boma la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga (EACOP).

Amesema mradi huo, umekamilika kwa asilimia 84 na manufaa lukuki yameshapatikana, ikiwemo ajira kwa wakazi wa Chongoleani 1,300, huku 2,000 wakiajiriwa kutoka Tanga.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments