Wednesday, December 10, 2025
spot_img
HomeBiasharaDkt. Samia: Tunajivunia haya kwenye kilimo

Dkt. Samia: Tunajivunia haya kwenye kilimo

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan amesema katika miaka mitano iliyopita, Serikali yake imeimarisha ushirika na kuinua sekta ya kilimo cha mazao mbalimbali ikiwemo kahawa.

Kwa mujibu wa Dk Samia, juhudi hizo zimechochea kupanda kwa bei ya kilo moja ya kahawa, kutoka Sh4,000 hadi Sh12,000 inayouzwa sasa kutoka kwa wakulima.

Dk Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumatano Oktoba 1, 2025 alipozungumza na wananchi wa Hai, mkoani Kilimanjaro katika mkutano wake wa kampeni za urais, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Mbali na zao la kahawa, amesema Serikali yake imekuza na kulea ushirika na kuuondoa katika mtazamo wa kuwa chaka la wizi na unyang’anyi kwa wakulima, sasa umegeuka kuwasimamia.

“Tumeujenga ushirika leo, tunaamini kuuachia ugawaji wa pembejeo za mbolea na pembejeo nyingine. Ushirika unafanya hiyo kazi na unagawa kwa wakulima wenzao,” amesema.

Ameeleza kwa sababu ushirika unaaminika sasa, amesema anatarajia kuukabidhi viwanda mbalimbali nani imani yake kuwa vitaendelezwa vema.

Mengine yaliyofanywa kwenye kilimo, amesema ni kujengwa kwa skimu za umwagiliaji na kutengeneza fursa kwa vijana kupitia mradi wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT).

“Miaka mitano iliyopita tumefanya kazi kweli kweli na kwa maana hiyo, napata ujasiri wa kusimama mbele yenu kuomba kura za CCM,” amesema.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments