Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeBiasharaWaziri Kikwete atembelea banda la NMB Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Mbeya

Waziri Kikwete atembelea banda la NMB Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Mbeya

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete, amezuru Banda la Benki ya NMB katika Maadhimisho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika kwenye viwanja vya Soko la Uhindini jijini Mbeya.

Katika ziara hiyo, Ridhiwani alipokelewa na Meneja Mahusiano wa Idara ya Wateja Binafsi, Luiana Keenja, pamoja na Meneja Mauzo Kanda ya Nyanda za Juu, Ungandeka Mwakatage. Waziri alipongeza juhudi za NMB katika kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia huduma za kifedha, mikopo na elimu ya fedha inayotolewa na benki hiyo katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza katika banda hilo, maofisa wa NMB walieleza kuwa benki hiyo inatumia maadhimisho hayo kutoa elimu ya fedha kwa vijana, kuwahamasisha kuhusu uwekaji akiba, pamoja na kuwaelimisha namna ya kupata mikopo ya ujasiriamali kupitia programu maalum za vijana na makundi yenye malengo ya maendeleo.

Aidha, Waziri Ridhiwani alihimiza taasisi za kifedha kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuunga mkono ajenda ya uwezeshaji vijana, hasa katika ujasiriamali na matumizi ya teknolojia za kidijitali ili kuongeza fursa za ajira na kipato kwa vijana nchini.

Benki ya NMB ilitumia maadhimisho hayo kutoa elimu ya fedha, ushauri wa uwekezaji, na kuwahamasisha vijana kuhusu fursa za mikopo ya ujasiriamali kupitia programu zake za uwezeshaji kijamii na kifedha.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments