Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeHabariSamia: Nitajenga SGR, kufufua bandari isiyotumika Mara

Samia: Nitajenga SGR, kufufua bandari isiyotumika Mara

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan amesema katika Mkoa wa Mara pekee, atafufua bandari zisizotumika, kufikisha mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) Mjini Musoma na kuuendeleza uwanja wa ndege.

Dk. Samia ametoa ahadi hizo leo, Alhamisi Oktoba 9, 2025 katika hotuba yake mbele ya wananchi wa Musoma, mkoani Mara, katika mkutano wake wa kampeni za urais.

Amesema anatambua kuna haja ya Mkoa wa Mara kuwa na Uwanja wa Ndege na kwamba atauendeleza ili ufikie kiwango cha kutua ndege kubwa za kibiashara.

Kuhusu bandari iliyoacha kutumika, amesema itafufuliwa na iliyopo itaendelezwa, ili MV Mwanza itakayosafirisha abiria na mizigo kutoka Mwanza hadi Mara na meli nyingine kubwa zitie nanga.

Dkt Samia pia ameahidi kujenga SGR kutoka Bandari ya Tanga, kupitia Moshi, Arusha hadi Musoma na inatarajiwa kuleta mapinduzi ya kiuchumi ndani ya mkoa huo.

“Ndugu zangu Wana Mara lililobaki hapa twendeni tukachague CCM ili tuliyoyasema hapa tukayafanyie kazi,” amesema.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments