Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan amewaonya baadhi ya makada wa chama hicho wanaowaunga mkono wagombea wa vyama vya upinzani, akisema wasitarajie CCM itashindwa.
Makada wanaozungumziwa na Dk Samia, ni baadhi ya waliokuwa watiania wa nafasi mbalimbali kwa tiketi ya chama hicho, lakini vikao havikuwapitisha.
Dk Samia ametoa onyo hilo leo, Alhamisi Oktoba 9, 2025 katika hotuba yake mbele ya wananchi wa Musoma mkoani Mara, katika mkutano wake wa kampeni za urais.
“Najua ndani ya Mara hapa kuna watu wamenunanua na katika kununa kwao wanasaidia wagombea wa vyama vya upinzani, ili waikomoe CCM.
“Tunataka kuwaambia CCM haikomoki na katika kuthibitisha hilo, niwaombe ndugu zangu Oktoba 29 tutoke wote kwa pamoja tukachague CCM,” amesema Dkt Samia.




