Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeHabariDkt Samia: Tukapige kura kuwezesha maendeleo

Dkt Samia: Tukapige kura kuwezesha maendeleo

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kujitokeza kupiga kura Oktoba 29, ili kuiwezesha Serikali kutafuta fedha ndani na nje ya nchi kwa ajili ya maendeleo.

Dk. Samia ametoa ahadi hiyo leo, Jumapili Oktoba 12, 2025 alipozungumza na wananchi wa Mbogwe mkoani Geita, katika mkutano wake wa kampeni za urais.

Amesema Oktoba 29, kila mwananchi aliyejiandikisha ahakikishe anakwenda kupiga kura, huku mabalozi wa mitaa wakipewa jukumu la kuwahamasisha wananchi wao.

“Nasema hivyo kwa sababu tunakwenda kukiheshimisha Chama Cha Mapinduzi, chama hiki kimefanya makubwa kwa nchi yetu, chama hiki kinakwenda kufanya makubwa kwenye nchi yetu,” amesema.

Ameeleza ni muhimu kupiga kura ili kuiwezesha Serikali kutafuta fedha ndani na nje ya nchi, kutekeleza miradi iliyoahidiwa.

Aidha, katika eneo hilo, ameahidi kutekeleza mradi wa Barabara ya Masungwe-Kasosobe yenye urefu wa kilomita 45 kuelekea Makao Mkuu ya Wilaya na kufikisha huduma za kijamii karibu na wananchi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments