Mashindano ya ngalawa yamesisimua Maadhimisho ya 44 ya Siku ya Chakula Duniani mkoani Tanga, yakishirikisha timu 12 kutoka maeneo mbalimbali.
Timu namba 010, inayoongozwa na Idd Kileo, ilinyakua ushindi kwa dakika 48:30, ikifuatiwa na timu za Amir Seleman na Mahamud Rashid.
Kaimu Mkurugenzi wa Mifugo, Nankondo Senzira, alisema mashindano hayo yanaonyesha mchango wa sekta ya uvuvi katika ajira na lishe bora.
Mwakilishi wa FAO, Charles Tulahi, aliongeza kuwa bahari ni hazina ya chakula, ajira na afya kwa Watanzania.




