Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeHabariHii ndio Misenyi chini ya Dk. Samia

Hii ndio Misenyi chini ya Dk. Samia

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan amesema katika miaka mitano ijayo, atajenga uwanja wa ndege wa kisasa, miradi tisa ya maji na barabara za kiwango cha lami, wilayani Misenyi katika Mkoa wa Kagera.

Kwa mujibu wa Dk Samia, anafanya hivyo akilenga kuinua maisha ya Watanzania wanaoishi wilayani humo na kuujenga utu wa mtu kama ilivyo kaulimbiu ya chama hicho ya Kazi na Utu, Tunasonga Mbele.

Samia ametoa ahadi hizo leo, Jumatano Oktoba 15, 2025 alipozungumza na wananchi wa Misenyi mkoani Kagera, katika mkutano wake wa kampeni za urais.

Miradi tisa hiyo ya maji, amesema inatarajiwa kunufaisha maeneo ya Bugango, Buchurago, Bubale, Minziro, Bugorora, Ruzinga, Bugandika, Mushasha, Mwemage, Byeju, Kashyenye, Kanyingo na Mgana.

Mradi mwingine ni kuweka lami kilomita mbili katika Barabara ya Bulembo Kona hadi Hospitali ya Wilaya na kukamilisha ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Buyango ili vijana wapate ujuzi utakaowawezesha kuajiriwa na kujiajiri.

Ujenzi wa soko la kisasa la Bunazi, mikopo kwa wananchi kwa ajili ya ufugaji wa samaki kwenye vizimba katika Mwalo wa Kabindi na kupeleka miche milioni mbili ya kahawa na 500,000 ya parachichi ni ahadi nyingine alizozitoa kwa wananchi wa Misenyi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments