Mgombea ubunge wa Jimbo la Mtama, Nape Moses Nnauye, amewaasa Watanzania kutokushawishika na kuingia kwenye ugomvi wa kisiasa, akisema kufanya hivyo ni hatari kwa amani na maslahi ya taifa.
Akizungumza katika programu yake maalum iitwayo “Kijiweni na Kaka Mkubwa”, Nape amesema lengo la mpango huo ni kuzungumza na wananchi wa makundi mbalimbali kuhusu masuala ya siasa, umoja na maendeleo ya nchi.
Amesema ni muhimu kwa Watanzania kuendelea kujadili tofauti zao kwa njia ya kistaarabu, badala ya kugombana au kuchochea migawanyiko ya kisiasa.
Kwa mujibu wa Nape, program hiyo ya “Kijiweni na Kaka Mkubwa” inalenga kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa siasa safi, inayojenga badala ya kubomoa, na kuchochea mshikamano wa kitaifa hasa katika kipindi cha uchaguzi.




