Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, ameendelea na mikutano ya kampeni kwa kishindo, ambapo leo Oktoba 18, 2025, amezungumza na umati mkubwa wa wananchi katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika Mpanda Mjini, mkoani Katavi.
Katika matukio mbalimbali ya picha yaliyonaswa wakati wa mkutano huo, Dk. Samia alionekana akiwahutubia wananchi kwa ari na matumaini, huku akisisitiza dhamira ya serikali ya CCM kuwaletea maendeleo endelevu, hususan katika sekta za elimu, afya, na miundombinu.




Wananchi wa Mpanda walijitokeza kwa wingi, wakionyesha mshikamano na uungwaji mkono kwa mgombea huyo ambaye pia ni Rais wa sasa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.








