Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeMichezoTimu ya Mlandege yazidi kutesa, Mafunzo hali mbaya

Timu ya Mlandege yazidi kutesa, Mafunzo hali mbaya

Timu ya Mlandege imeendeleza ubabe wake baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya New Stonetown katika mchezo wa Ligi Kuu Zanzibar uliochezwa juzi jioni, huku Mafunzo FC ikiendelea kupoteza mwelekeo.

Katika mechi nyingine, Mafunzo ilikubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa KVZ FC kwenye Uwanja wa Mau A, ikiwa ni mchezo wao wa tano wa msimu huu.
Kwa matokeo hayo, Mafunzo imebaki na pointi tano pekee, ikiwa imeshinda mechi moja, kutoka sare mbili na kupoteza michezo miwili.

Kocha Mkuu wa Mafunzo, Haji Nuhu, alisema changamoto wanazokutana nazo ni zao la ongezeko la ushindani katika ligi hiyo.
“Ligi Kuu Zanzibar imekuwa ngumu sana kwa sasa, kila timu imejiimarisha vizuri katika usajili na makocha wengi wanafanya kazi kwa ubora wa hali ya juu,” alisema.

Aliongeza kuwa makosa katika eneo la ulinzi yameigharimu timu yake.
“Mabao yote tuliyoruhusu yametokana na kukosa umakini wa mabeki. Tulijaribu kutumia mbinu ya kuzuia zaidi na kushambulia kwa kushtukiza, lakini haikufanikiwa kama tulivyotarajia,” alisema Nuhu, akibainisha kuwa anatarajia kufanya marekebisho kuelekea michezo ijayo.

Kwa upande wake, Kocha Msaidizi wa Mlandege, Sabri China, alisema ushindi huo ulikuwa matokeo ya nidhamu, ari na kujituma kwa wachezaji wake.
“Tumepata ushindi wa kwanza msimu huu na kwa ugenini, jambo hili limeongeza morali ya wachezaji kuelekea mechi zijazo,” alisema China.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments