Rais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema vijana wengi waliokamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya uhaini hawakujua walichokifanya, hivyo amevielekeza vyombo vya sheria kuangalia kiwango cha waliyoyafanya.
Dk. Samia ametoa kauli hiyo, leo Ijumaa Novemba 14,2025 wakati akihutubia Bunge jijini Dodoma, ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Bunge la 13, ambapo pamoja na mambo mengine alitoa mwelekeo wa Serikali yake kwa miaka mitano ijayo.
“Nikiwa kama mama na mlezi wa Taifa, ninavielekeza vyombo vya sheria hasa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka kuangalia kiwango cha makosa yaliyofanya na vijana wetu.
“Kwa wale wanaonekana wamefuata mkumbo, lakini hawakuonekana na dhamira ya kufanya uahalifu, wawafutie makosa yao.Pia walionekana kufuata mkumbo, lakini hawakudhamilia kufanya uhalifu, wawafutie makosa yao,”




