Mwanasoka wa zamani wa Taifa Stars, Boniface Pawasa, amewataka wachezaji kutuliza akili na kuongeza umakini wanapojiandaa na AFCON Morocco, licha ya kupoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kuwait.
Amesema timu ilionesha ushindani na anashauri wachezaji kuwa na mawasiliano mazuri uwanjani ili kuepuka makosa rahisi. Pia amempongeza Kocha Miguel Gamondi kwa kikosi alichokiita na kumtaka kuendelea kuboresha mapungufu aliyoyaona.




