Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake ya ACT Wazalendo, Janeth Rithe amelaani vikali kitendo cha Jeshi la Polisi kumkamata Katibu wa Baraza la Wanawake la CHADEMA, Pamela Maasay na makada wengine wa Chama hicho wilayani Musoma.
Rithe amesema ni jambo lisilokubalika kwa Jeshi la Polisi kutumia nguvu kwa mabomu ya machozi katika viunga vya Kanisa kwa ajili ya kuwakamata wanachama wa CHADEMA waliokuwa wanahudhuria misa kanisani.Â
Rithe ametoa kauli hiyo kwenye kikao na viongozi wa Ngome ya Wanawake katika Jimbo la Tunduru Kaskazini kilichofanyika katika Kijiji cha Namasakata leo Machi 09, 2026.Â

Kikao hicho ni mwendelezo wa ziara ya Ngome hiyo katika maeneo mbalimbali nchini inayolenga kuzifariji familia zilizokubwa na madhila kutokana na matukio ya Oktoba 29, 2025.
Katika hatua nyingine Rithe ametuma salamu za mshikamano kwa Mwenyekiti wa BAWACHA,Sharifa Suleiman na kusisitiza kuwa ACT Wazalendo itashirikiana na wapenda demokrasia wote katika kupigania demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria nchini.





