Mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu Ado amesema wabunge walio wachache bungeni wanamkopesha imani Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba kwa matarajio kuwa atajikita katika kusimamia rasilimali za Taifa kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo, kuipatia nchi katiba mpya na kushughulikia changamoto za kiuchumi na kijamii za wananchi.
Ado ameyasema hayo leo Novemba 13,2025 alipotakiwa na Spika Hassan Zungu kutoa neno kwenye uteuzi wa Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania uliofanya na Rais Samia Suluhu Hassan.




