Wednesday, March 11, 2026
spot_img
HomeHabariAdo Shaibu: Tutampigania Mpina hadi hatua ya mwisho

Ado Shaibu: Tutampigania Mpina hadi hatua ya mwisho

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu amesema Chama hicho kitalifuatilia suala la kutoteuliwa kwa Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama hicho Luhaga Mpina hadi arejeshwe kwenye kampeni na kupigiwa kura.

Ado ameyasema hayo kwenye Mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Chama hicho katika Jimbo la Tunduru Kusini.

“.. Kwenye hili la kutoteuliwa kwa Ndugu Mpina, sisi msimamo wetu ni kuwa it’s not over until it’s over. Haijaisha mpaka iishe. Sisi tutapambana kwa njia zote ili mgombea wetu arejeshwe na aweze kuteuliwa na kupigiwa kampeni na kura. Kwa sasa suala hili lipo mahakamani na tunaiachia mahakama ilishughulikie” amesisitiza Ado.

Katika hatua nyingine Ado amemnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya ACT Wazalendo Ndugu Mtutura Abdallah Mtutura na kuwaomba wananchi wamchague kwa kura nyingi kwa sababu alipokuwa Mbunge wa Jimbo hilo alifanya mengi mazuri kwa ustawi wa Tunduru.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments