Saturday, March 21, 2026
spot_img
HomeMichezoAjali Nigeria yamlazimisha Anthony Joshua kuachana na ndondi

Ajali Nigeria yamlazimisha Anthony Joshua kuachana na ndondi

Mmoja wa wanafamilia wa bondia maarufu Anthony Joshua amedai kuwa nyota huyo wa ndondi ameamua kustaafu rasmi mchezo huo kufuatia ajali mbaya ya barabarani iliyotokea nchini Nigeria.

Joshua (36) alihusika katika ajali ya kutisha Jumatatu iliyopita kwenye barabara ya Lagos–Ibadan, eneo la Makun, baada ya gari alilokuwa akisafiria kugongana na lori lililokuwa limesimama kando ya barabara. Ingawa bondia huyo alipata majeraha madogo, marafiki wake wa karibu na wajumbe wa timu yake, Sina Ghami na Latif “Latz” Ayodele, walifariki dunia papo hapo.

Mazishi ya wawili hao yalifanyika Jumapili, Januari 4, katika msikiti mmoja jijini London, ambapo Joshua alihudhuria kutoa heshima za mwisho kwa waliokuwa wakifanya kazi naye kwa ukaribu.

Ajali hiyo ilitokea siku 10 tu baada ya pambano lake la hivi karibuni, ambapo Joshua alimchapa Jake Paul kwa knock-out katika pambano lililofanyika Miami, Marekani, tarehe 19 Desemba.

Hadi sasa, Anthony Joshua hajazungumza hadharani kuhusu mustakabali wake katika mchezo wa ndondi. Aidha, promota wake Eddie Hearn pamoja na kampuni ya Matchroom Boxing wamekataa kutoa maelezo zaidi, wakibaki na taarifa ya awali iliyotolewa usiku wa tukio hilo.

Hata hivyo, mjomba wake, Adedamola Joshua, ameliambia gazeti la The Punch kuwa bondia huyo tayari ameweka wazi uamuzi wake wa kustaafu ndondi, akitaja mshtuko mkubwa wa ajali hiyo kama sababu kuu ya uamuzi huo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments