Wednesday, March 11, 2026
spot_img
HomeHabariRaia wa Kichina wakamatwa Oysterbay na zaidi ya bilioni 6 taslimu

Raia wa Kichina wakamatwa Oysterbay na zaidi ya bilioni 6 taslimu

Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Oysterbay, chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, umefanikiwa kuwabaini raia wa kigeni wenye asili ya Kichina waliokuwa wakiishi katika Apartments za Phoenix, Mtaa wa Mazengo, Oysterbay.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya uongozi kubaini mwenendo wa maisha usio wa kawaida, ikiwemo matumizi makubwa ya fedha yasiyoendana na shughuli halali za kibiashara. Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakiingia na kutoka nyakati za usiku kuanzia saa 7:30 hadi alfajiri, wakitumia magari mbalimbali na kubeba mafurushi kila siku.

Baada ya kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, operesheni maalum ilifanyika leo majira ya saa 5:30 asubuhi na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao. Katika upekuzi uliofanyika kwenye Apartment namba 317, ghorofa ya tatu, ilibainika kuwepo fedha taslimu zaidi ya shilingi bilioni 6 zilizokuwa zimefichwa, fedha ambazo zinadaiwa kuwa na uhusiano na shughuli zisizo halali.

Uchunguzi zaidi unaendelea.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments