Tuesday, March 31, 2026
spot_img
HomeHabariAjali ya basi yaua watu 6, yajeruhi 55

Ajali ya basi yaua watu 6, yajeruhi 55

Watu sita wamefariki dunja na wengine 55 wamejeruhiwa baada ya basi waliyokuwa wakisafiria kutoka Dodoma kwenda Mwanza kuanguka na kupinduka kufuatia tairi la mbele kupasuka baada ya kugonga shimo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Amon Kakwale, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotolea leo saa 4:00 asubuhi, hata hivyo hakueleza kwa kina kwasababu alikuwa bado yupo eneo la tukio.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,Thomas Apson, akizungumza na waandishi alisema ajali hilo ambayo imehusisha basi la kampuni ya Green Line yenye namba za usajiri T 689 DCN, imetokea katika kijiji cha Mkiwa wikaya ya Ikungi mkoani Singida.

Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wikaya ya Manyoni, Dk. Bwire James, alisema hospitali hiyo imepokea majeruhi 55, kati yao wanaume ni 34 na wanawake ni 21 na maiti 6.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments