Friday, April 3, 2026
spot_img
HomeAfyaAmref Tanzania yaongeza uelewa kuhusu usonji

Amref Tanzania yaongeza uelewa kuhusu usonji

Katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uelewa wa Usonji (Autism), yenye kauli mbiu “Weka Tumaini Usoni Mwao: Amref Health Africa Tanzania imeungana na Wizara ya Afya Tanzania kuongeza uelewa na kuimarisha huduma kwa watoto wenye usonji (ASD).

Kupitia mradi wa Shining a Light on Autism, Amref inaendelea kujenga uwezo wa wahudumu wa afya katika tiba ya Occupational Therapy ili kuboresha utambuzi wa mapema, usimamizi na utoaji wa huduma kwa watoto wenye hali hiyo.

Maadhimisho hayo yaliandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Afya, Amref Tanzania na Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe kwa ufadhili wa NBC Tanzania. Tukio hilo lilifanyika jijini Dodoma likihusisha wahudumu wa afya na wanufaika mbalimbali kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu usonji katika jamii.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dan Bwana, Meneja wa Mradi kutoka Amref Tanzania, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kuimarisha huduma jumuishi za afya.

Amesema kupitia ufadhili wa NBC Tanzania, Amref inaendelea kuwawezesha wahudumu wa afya wa ngazi ya jamii kwa kuwapatia ujuzi muhimu, hatua inayochangia upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wote bila kumuacha mtu yeyote nyuma.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments