
MADRID, Hispania
CARLO Ancelotti, amedai Real Madrid haikustahili kuchapwa vikali hivyo na Barcelona kwenye El Clasico Jumamosi usiku na kutoa ukumbusho wa mafanikio ya awali ya timu yake, licha ya kushindwa vibaya.
Barcelona walipata ushindi wao wa kwanza ugenini kwenye Uwanja wa Bernabeu tangu mwaka 2022, huku mabao mawili ya Robert Lewandowski yakikishangaza kikosi hicho kilichokuwa nyumbani.
Lamine Yamal na Raphinha waliongeza mabao mawili zaidi na kufanya safu ya mabao kuwa mbaya sana kwa Madrid, ambao sasa wako pointi sita nyuma ya wapinzani wao hao wakubwa katika mbio za ubingwa wa LaLiga.
Ina maana ‘Los Blancos’ wana kazi nyingi ya kufanya, ili kutetea ubingwa, lakini Ancelotti alikuwa mwepesi kuwatetea wachezaji wake na kuangazia njia yao ngumu ya kupata utukufu siku za nyuma.
Alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari, baada ya mechi: “Matokeo hayaakisi kile kilichotokea. Walistahili kushinda lakini ulikuwa mchezo wetu.
“Tunapaswa kujifunza kutokana na hili. Kujikosoa ni jambo la msingi. Lakini hatutupi kila kitu kwenye pipa – kipindi chetu cha kwanza kilikuwa kizuri.
“Mara ya mwisho tulipoteza 4-0 nyumbani kwa Barcelona, tulishinda LaLiga na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hatutaacha kupigana.”
Madrid wameshindwa kusonga mbele licha ya kumuongeza Kylian Mbappe kwenye kikosi chao wakati wa majira ya joto na walihitaji ufufuo wa kipindi cha pili, ili kuifunga Borussia Dortmund katika Ligi ya Mabingwa katikati ya wiki.
Mbappe alitatizika katika mechi yake ya kwanza ya El Clasico, akipotea kwa kuotea mara nane, huku Vinicius Junior, akikosa nafasi nzuri katika kipindi cha kwanza.