Arteta: Arsenal iko hai kwa mbio za ubingwa

LONDON, England

KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, amepunguza umuhimu wa pengo la pointi tano kwa vinara wa Ligi Kuu England Manchester City kwa kusifia timu yake kuwa hai katika mbio za ubingwa baada ya sare ya mabao 2-2 na Liverpool Jumapili.

Bukayo Saka alifunga bao la kuongoza likiwa lake la 50 la ligi baada ya dakika tisa kabla ya Virgin van Dijk kusawazisha kwa kichwa dakika ya 18.

Mikel Merino alifunga kwa kichwa mpira wa adhabu wa Declan Rice na kurejesha uongozi wa ‘Washikabunduki’, kabla ya kipindi cha mapumziko, lakini bao la kusawazisha la Mohamed Salah la dakika ya 81 liliokoa pointi moja kwa Liverpool.

Liverpool wanasalia katika nafasi ya pili, pointi nne mbele ya Arsenal ambao wanashika nafasi ya tatu huku City wakifurahia kileleni wakati huu wakisaka taji la tano mfululizo.

Alipoulizwa jinsi tofauti ya pointi katika hatua hiyo ya mwanzo ya msimu, Arteta alisema: “Hutaki kuwa katika nafasi hiyo. Unataka kuwa mbele kwa pointi tano, lakini hapa ndipo tulipo. Timu iko hai.

“Wanaojeruhiwa, waliopo wapo katika wakati mzuri. Mambo yatatokea na tunaenda kuwa mahali pazuri zaidi.

“Naona timu na sina mashaka, nadhani nilikuambia siku tatu kabla kwamba tutapanda ndege Jumapili na tulianza kuruka na tulikuwa timu bora zaidi.

“Tulihitaji kupata pointi leo (juzi) ili kutafakari tulipo na tunapotaka kuwa. Hatukuweza kufanya hivyo lakini kwa uhakika tupo.”

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *