Wednesday, March 11, 2026
spot_img
HomeMichezoAwesu, Chasambi karibu kutua JKT Tanzania

Awesu, Chasambi karibu kutua JKT Tanzania

Klabu ya JKT Tanzania ipo kwenye mazungumzo na Simba SC kwa ajili ya kuwapata wachezaji Ladack Chasambi na Awesu Awesu.

Inadaiwa kuwa dili hilo litahusisha kubadilishana na wachezaji wa Simba, kipa Yacoub Suleiman na beki Wilson Nangu, pamoja na kiasi cha fedha.

Awali mazungumzo hayo yalionekana kugonga mwamba, lakini Simba wamerudi tena na kuonesha nia ya dhati ya kuwapata nyota hao.

Taarifa zinasema uongozi wa Simba tayari umekubaliana, ingawa bado unasubiri baraka za kocha Fadlu Davids, ambaye Yacoub na Nangu ni miongoni mwa chaguo lake.

Kwa upande mwingine, JKT Tanzania tayari imesajili wachezaji wapya akiwemo Paul Peter (Dodoma Jiji), Laurian Makame (Fountain Gate) na kipa Ramadhani Chalamanda (Kagera Sugar), anayetarajiwa kuchukua nafasi ya Yacoub. Kikosi hicho kipo kambini Arusha kikijiandaa kwa msimu mpya.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments