📌Huu ukiwa ni mkakati wa Global Gateway wa Umoja wa Ulaya kuunga mkono uwekezaji wa huduma ya intaneti nchini Tanzania na Madagascar.
📌Mradi huu unatarajiwa kuongeza zaidi ya mara mbili ueneaji wa mtandao wa 4G nchini Madagascar na Tanzania na kuendeleza zaidi usambazaji wa teknolojia ya 5G.
Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (European Investment Bank Global) leo imetangaza ufadhili wa dola za Kimarekani milioni 100 kwa AXIAN Telecom (Kampuni mama ya Yas) kwa lengo la kusaidia upanuzi wa miundombinu ya huduma za intaneti nchini Tanzania na Madagascar.

Mradi huu unalenga kuimarisha upatikanaji wa huduma za 4G na kuendeleza usambazaji wa teknolojia ya 5G.
Uwekezaji huu mpya kupitia mpango wa Global Gateway, ambao unaungwa mkono na dhamana ya bajeti ya Tume ya Ulaya, utaboresha upatikanaji wa huduma ya intaneti, kuhimarisha ujumuishi wa kidigitali na kuchochea maendeleo endelevu katika nchi hizi mbili.
Pia, uwekezaji huu utasaidia kupunguza tofauti za kijiografia katika upatikanaji wa huduma za mawasiliano barani Afrika na masoko yanayochipukia.
AXIAN Telecom ni Kampuni inayoongoza barani Afrika katika utoaji wa huduma za mawasiliano, yenye nafasi thabiti sokoni katika maeneo muhimu ambapo huduma zake zinapatikana.
Kwa sasa AXIAN Telecom inahudumia zaidi ya wateja milioni 44 na inaendesha shughuli zake katika nchi tisa zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara, ikiwemo:-Tanzania, Madagascar, Senegal, Togo na Visiwa vya Comoro.
Katika fedha hizi, Tanzania itapokea dola milioni 60 za Kimarekani, huku Madagascar ikipokea dola milioni 40.
AXIAN Telecom inamiliki chapa ya Yas katika nchi hizi zote mbili.Mkurugenzi Mtendaji wa AXIAN Telecom, Bw. Hassan Jaber alisema: “Ufadhili huu wa dola milioni 100 kutoka EIB Global utatusaidia kuboresha miundombinu huduma za intaneti nchini Madagascar na Tanzania na kuwafaidisha mamilioni ya wananchi.
Uwekezaji huu mkubwa kwenye mtandao utafungua njia ya ukuaji wa kijamii na kiuchumi, ujumuishaji wa kidigitali na fursa bora kwa wote.””Uunganishwaji wa kidijitali hufungua milango ya elimu, biashara, huduma za afya na ujumuishwaji wa kijamii,” alisema Makamu wa Rais wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, Ambroise Fayolle.
“Uwekezaji huu mpya unaonyesha dhamira ya European Investment Bank katika kuwawezesha wananchi, kuendeleza maendeleo endelevu, na kuleta mabadiliko chanya kupitia upatikanaji wa mawasiliano kwa bei nafuu.”
Kuimarika kwa uunganishwaji wa mawasiliano kuna mchango mkubwa katika kusukuma maendeleo ya kijamii na kiuchumi, na uwekezaji huu chini ya mkakati wa Global Gateway wa Umoja wa Ulaya unaenda sambamba na malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ya Umoja wa Kimataifa. Kupitia upanuzi wa miundombinu ya huduma ya intaneti iliyo imara na yenye ufanisi.
Uwekezaji mpya wa EIB Global utafungua fursa nyingi zinazohusiana na malengo endelevu (SDGs) ikiwemo kukuza uchumi wa viwango vya juu kwa njia jumuishi na endelevu, hali itakayochochea uundwaji wa ajira bora.

Jamii zilizo katika mazingira magumu zitapata nyenzo na rasilimali muhimu zitakazowawezesha kuunganishwa na dunia kwa upana zaidi, hivyo kukuza ushirikishwaji wa maarifa, biashara mtandaoni, na ubunifu.
Mabalozi wa Umoja wa Ulaya nchini Madagascar na Tanzania wameelezea kuunga mkono kwao uwekezaji wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) pamoja na athari chanya za uwekezaji huo katika kuendeleza maendeleo ya nchi hizo.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Madagascar na Muungano wa Visiwa vya Comoro, Roland Kobia, alisema, “Ahadi hii kutoka Umoja wa Ulaya kupitia European Investment Bank inaonyesha dhamira yetu ya kuchangia maendeleo endelevu ya Madagascar kupitia uwekezaji wa sekta binafsi, ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kufungua fursa kwa wote.
Uwekezaji huu utaimarisha huduma ya intaneti yenye kasi kwa njia ya simu (mobile broadband) na kuleta fursa muhimu za ukuaji wa kiuchumi na kijamii katika maeneo yote ya Madagascar.
Upanuzi wa 4G na usambazaji wa teknolojia ya 5G katika mazingira ya ushindani wa haki baina ya watoa huduma za mawasiliano utakuwa chachu ya ujumuishaji kidijitali, huku ukisaidia elimu, ubunifu na uundaji wa ajira mpya.
”Kwa upande wake, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bi. Christine Grau, alisema, “Umoja wa Ulaya ni mshirika muhimu wa Tanzania katika kusukuma mbele ajenda ya Serikali ya mageuzi ya kidijitali.
Ushirikiano wetu ni mpana, ukihusisha usaidizi wa kisera pamoja na uwekezaji kwenye miundombinu. Uwekezaji huu wa EIB Global kwa AXIAN Telecom, unaowezeshwa kupitia dhamana ya Umoja wa Ulaya, ni mfano halisi wa dhamira yetu ya kuwekeza katika uunganishwaji wa kidijitali.
Umoja wa Ulaya unaamini kuwa katika eneo la uunganishwaji wa mawasiliano, kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi ni muhimu ili kufanikisha mabadiliko ya kidijitali yanayomlenga kila mwananchi na kuhakikisha hakuna anayebaki nyuma.
”EIB Global ni mfadhili mkubwa katika sekta ya mawasiliano na mabadiliko ya kidijitali barani Afrika na katika masoko yanayochipukia.
Mradi huu unaunga mkono malengo ya mpango wa Umoja wa Ulaya wa Digital4Development (D4D) uliozinduliwa mwaka 2017.
Pia unaendana na Mkakati wa Global Gateway kwa Afrika, unaolenga kuchochea uwekezaji wa hadi euro bilioni 150 ifikapo mwaka 2030 kwa ajili ya maendeleo ya miundombinu ya maeneo halisi na ya kidijitali katika bara lote la Afrika.
Kupitia ushirikiano na wadau wa ndani, watoa huduma za mawasiliano na mashirika ya serikali, EIB Global inalenga kujenga mfumo wa kidijitali ulio jumuishi na shirikishi. Ingawa AXIAN Telecom inafanya kazi katika soko lenye ushindani mkubwa, ongezeko la idadi kubwa la vijana katika nchi inazofanyia shughuli linatarajiwa Ingawa AXIAN Telecom inafanya kazi katika soko lenye ushindani mkubwa, ongezeko la idadi ya vijana katika nchi ambazo kampuni hiyo inatoa huduma inatarajiwa kuchochea kwa kasi ukuaji wa mahitaji ya mawasiliano ya simu na huduma za kidijitali.