Azam FC yamkabidhi Ibenge dhamana ya kuvunja rekodi CAF

Azam FC imesema moja ya uwekezaji bora msimu huu ni kumsajili kocha nyota wa DR Congo, Florent Ibenge, ikiamini ataifikisha timu hiyo kwa mara ya kwanza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Ofisa Habari wa Azam, Hasheem Ibwe, alisema matumaini hayo yameongezeka baada ya droo kuipanga Azam kuanzia ugenini dhidi ya Al-Merreikh Bentiu ya Sudan Kusini, Septemba 19, kabla ya kurudiana Dar es Salaam Septemba 26.

Ibwe alisema ingawa hawajui mengi kuhusu wapinzani hao, wanaamini Azam iliyoboreshwa chini ya Ibenge inaweza kufanya vizuri zaidi kuliko misimu iliyopita.

Ibenge amewahi kufundisha AS Vita ya DR Congo, RS Berkane (akiwaipa Kombe la Shirikisho) na Al Hilal ya Sudan, aliyoipeleka robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ibwe aliongeza kuwa licha ya baadhi ya timu kuonekana dhaifu, hawatodharau mpinzani yeyote.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *