Azam FC yamwekea Ibenge masharti ya Pointi 70

Klabu ya Azam FC imesema kocha wao mpya, Florent Ibenge, anatakiwa kuvunja rekodi za msimu uliopita kwa kukusanya angalau pointi 70 na kuifikisha timu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Mkuu wa Habari wa klabu hiyo, Thabit Zacharia ‘Zaka’, alisema hawajamlazimisha Ibenge kushinda ubingwa, bali wanataka maendeleo ya kweli kwenye uwanja wa matokeo. Alibainisha kuwa Azam haijawahi kufikisha pointi 70 katika historia ya Ligi Kuu, hivyo lengo la msimu huu ni kuvuka kiwango hicho.

Aidha, Zaka alisisitiza kuwa mafanikio ya kweli hayapimwi kwa mataji pekee bali kwa hatua za maendeleo, huku akisema pia wanataka kuvuka hatua ya awali kwenye mashindano ya kimataifa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *