Klabu ya Azam imeeleza ugumu ilioupata katika kumsajili kipa Issa Fofana kutoka Al Hilal ya Sudan, pamoja na wachezaji wawili wa Tunisia, Baraket Hmidi na Ben Zitoune Tayeb.

Mkuu wa Habari wa Azam, Thabit Zacharia alisema wachezaji kutoka Afrika Kaskazini mara nyingi husita kuja kucheza Tanzania kutokana na mazingira mapya wasiyozoea.
Fofana, ambaye aliisaidia Al Hilal kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita, alichelewa kuachwa na klabu yake.
Azam pia imepata saini ya Baraket aliyekuwa CS Sfaxien na Tayeb, beki kutoka Al Hilal, ambaye pia ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao.


