Sunday, December 7, 2025
spot_img
HomeHabari‘Banda la Mama’ yaomba vijana na Watanzania wote kumnadi Samia

‘Banda la Mama’ yaomba vijana na Watanzania wote kumnadi Samia

Dar es Salaam
Mratibu wa kampeni ya “Banda la Mama”, Mhandisi Aivan Maganza, amewataka Watanzania, hususan vijana wa vyama vyote vya siasa, kuhakikisha wanamtafutia ushindi mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, katika uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mhandisi Maganza alisema lengo la “Banda la Mama” ni kuhakikisha Dk. Samia anapata ushindi wa kati ya asilimia 80 hadi 100, kutokana na kazi kubwa na mafanikio aliyoyapata katika kipindi cha uongozi wake.

“Kampeni hii haina mrengo wa kisiasa, bali ni jukwaa la kuonyesha utambuzi wa wananchi kwa juhudi na maendeleo yaliyofanywa na Rais Samia katika kuimarisha ustawi wa taifa,” alisema Maganza.

Ameongeza kuwa vijana wanapaswa kuendelea kulipenda taifa lao, kulinda amani na kutumia Oktoba 29 kushiriki uchaguzi kwa amani, wakishindana kwa hoja na si kwa vurugu, wakitambua kuwa Tanzania ni nchi yao pekee.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments