Klabu ya Coastal Union imekamilisha usajili wa beki wa kati Mkenya, Christopher Oruchum, kutoka Pamba Jiji FC, pamoja na kiungo Mtanzania Khleffin Salum Hamdoun kutoka Muscat Club ya Oman.

Usajili huu unalenga kuimarisha kikosi kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu.
Coastal Union, iliyomaliza nafasi ya nane msimu uliopita, itaanza ligi Septemba 17 dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.




