Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Maji Mpanda yachota maarifa MUWSA

Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Menejimenti ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika Manispaa ya Mpanda wamefanya ziara mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, kwa lengo la kujifunza mbinu bora za uendeshaji wa mamlaka za maji.

Katika ziara hiyo, takribani watumishi 15 walitembelea Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) kujionea utekelezaji wa miradi ya maji na mifumo ya uendeshaji wa mamlaka hiyo.

Akizungumza wakati wa kuwapokea, Mkurugenzi Mtendaji wa MUWSA, Mhandisi Kija Limbe, alieleza mambo muhimu yanayochangia mafanikio ya mamlaka hiyo, huku akisisitiza umuhimu wa usimamizi thabiti wa rasilimali na teknolojia katika kuboresha huduma za maji safi na usafi wa mazingira.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mpanda, Martin Mwakabende, pamoja na Kaimu Mkurugenzi wake, Rehema Nelson, walieleza kuwa lengo la ziara yao ni kupata uzoefu wa namna bora ya kuendesha mamlaka yao kwa ufanisi zaidi.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Albert Msovera, alisema kuwa MUWSA ni miongoni mwa mamlaka zinazopaswa kuigwa, hivyo ziara hiyo imelenga kukuza ubunifu na kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa Mamlaka ya Maji Mpanda kwa kujifunza kutoka kwa wenzao wa Moshi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *