Nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, anaendelea kuthibitisha kwa vitendo kwa nini ni mhimili muhimu wa kikosi cha Manchester United msimu huu.
Kiungo huyo amehusika moja kwa moja katika mabao 12, akifunga mabao matano na kuongoza ligi kwa kutoa asisti saba. Aidha, ndiye mchezaji aliyeunda nafasi nyingi zaidi za mabao, akifikisha nafasi 50, jambo linaloonesha mchango wake mkubwa katika safu ya ushambuliaji.
Licha ya mchango huo mkubwa kila wiki, Manchester United imekuwa ikipitia nyakati ngumu na kushindwa kuonyesha kiwango cha kuridhisha kama timu, hali ambayo imefanya jina la Bruno Fernandes kutopewa uzito unaostahili ikilinganishwa na kiwango anachokionesha uwanjani.
Hata hivyo, takwimu zake zinaendelea kuthibitisha kuwa yeye ni mhimili wa mchezo wa United na mchezaji muhimu ambaye mchango wake haupaswi kupuuzwa.




