Timu ya soka ya Mamlaka ya Maji Bunda (BUWSSA) imekabidhiwa vifaa, maji na fedha na wadau wa maendeleo ili kushiriki michuano ya Maji Cup inayoendelea jijini Tanga.

Mkurugenzi Esther Gilyoma alisema mashindano hayo yana lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya wafanyakazi wa sekta ya maji.
Nahodha George Milanzi alisema timu yao imejiandaa vyema na misaada waliyopewa imeongeza morali. BUWSSA ilitarajiwa kumenyana na Mamlaka ya Maji Korogwe na inalenga kutwaa ubingwa.