Timu ya Singida Black Stars (BS) imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya CECAFA Kagame Cup baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC FC kwenye mchezo uliochezwa jijini Dar es Salaam.
Mabao ya ushindi yalifungwa na nyota wapya wa timu hiyo, Clatous Chama pamoja na Andy Kofi, na kuipeleka Singida BS hatua ya fainali.
Katika mchezo wa fainali, Singida Black Stars itakutana na Al Hilal ya Sudan, huku APR na KMC zikitarajiwa kukutana katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu. Mechi zote zitapigwa siku ya Jumatatu, Septemba 15.





