Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, CP Salum Hamduni, ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) mkoani humo, kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni, na mwongozo wa uratibu na usimamizi wa mashirika hayo, huku wakilinda maslahi ya taifa na kuheshimu mila na desturi za Mtanzania.

Amebainisha hayo leo Julai 30,2025 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, kwenye Mkutano wa Mwaka wa Mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani humo, wenye kauli mbiu isemayo,Tathimini ya miaka mitano ya mashirika yasiyo ya kiserikali katika maendeleo ya Taifa,Mafanikio, Changamoto na Fursa.
Amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika kusaidia jamii kupitia sekta mbalimbali, lakini akasisitiza umuhimu wa kuyatekeleza majukumu yao kwa uwazi, uadilifu, na utii wa sheria, bila kuruhusu kutumika kinyume na maslahi ya nchi.
“Serikali inatambua na kuthamini mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika kusaidia jamii, hivyo nawaomba katika utekelezaji wa majukumu yenu lindeni Maslahi ya nchi pamoja na kuheshimu mila na desturi za Mtanzania,”amesema CP Hamduni.
Aidha,ameyataka mashirika hayo pia, kuhakikisha wanawasilisha vibali vya utekelezaji wa miradi katika Mamlaka husika kipindi wanapopata miradi mipya, kuwasilisha taarifa za robo mwaka na mwaka ili kuwezesha zoezi la ufuatiliaji na tathimini,kuzingatia misingi ya uwajibikaji wa fedha za miradi,na kuzingatia vipaumbe,e vya serikali katika mipango yao.

Naye Afisa Maendeleo wa Mkoa wa Shinyanga Bestina Gunje.amesema mkoa huo una mashirika 206 na kwamba Mkoa huo wamekuwa wakishirikiana nayo kwa ukaribu katika kutekeleza Afua mbalimbali zinazogusa jamii hasa katika Sekta ya Maji,Afya,Elimu,Kilimo,Ufugaji,kupinga ukatili wa kijinsia,na uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Aidha,ametaja changamoto ambazo hukabiliana na mashirika hayo kuwa ni baadhi kutekeleza miradi bila kutoa taarifa Ofisi ya Mkoa,kuchelewa au kushindwa kuwasilisha taarifa za utekelezaji kwa Msajili wa Mashirika, pamoja na kutohuisha taarifa zao katika mfumo wa Nis mfano mtu mmoja kuwa na mashirika zaidi ya moja na kusababisha kupunguza umakini.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NaConGO) Mkoa wa Shinyanga Bakari Juma,akisoma Risala ya Mashirika hayo,amesema wanaahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika utoaji wa huduma mbalimbali kwa jamii.