Beki mkongwe Andrew Vicent ‘Dante’, aliyemaliza mkataba na KMC, yuko kwenye mazungumzo ya kujiunga na Kagera Sugar, ambayo msimu ujao itashiriki Ligi ya Championship baada ya kushuka daraja.

Licha ya kushuka, viongozi wa Kagera Sugar wapo kwenye mikakati ya kuunda kikosi imara chenye uzoefu ili kurudi Ligi Kuu msimu wa 2026/27.
Dante, ambaye aliibukia Mtibwa Sugar mwaka 2011 kabla ya kuchezea Yanga na klabu nyingine, anatarajiwa kuongeza uzoefu mkubwa kikosini.




