Thursday, March 5, 2026
spot_img
HomeHabariDAWASA bega kwa bega na wenyeviti wa mitaa uboreshaji huduma

DAWASA bega kwa bega na wenyeviti wa mitaa uboreshaji huduma

Dar es Salaam

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imewashirikisha wenyeviti wa mitaa ya Ulongoni, Kanga, Kichangani, Kwalimbanga, Sabasaba, Kinyerezi, Mongola Ndege, Kitunda na Kibaga katika utekelezaji wa zoezi la kubadilisha mabomba chakavu takribani 180 yenye ukubwa wa inchi 8 kila moja.

Zoezi hilo limetekelezwa kwa lengo la kuweka juhudi za pamoja za kuboresha huduma ya Majisafi pamoja na kuongeza uelewa juu ya jitihada za kupunguza kiasi cha maji kinachopotea.

Meneja wa DAWASA -Kinyerezi, Roberts Mugabe amesema zoezi hilo la kubadilisha miundombinu linahusisha kubadilisha bomba kwa umbali wa kilomita 2.16 ambapo linalenga kuongeza wingi wa maji katika maeneo hayo na kupunguza kiwango kinachopotea.

“Tunaamini viongozi ni chachu katika utoaji huduma za Maji, hivyo ushirikiano huu unalenga kurahisisha utoaji wa taarifa zinazohusu huduma zetu na kujenga uelewa wa pamoja” amesema Roberts

Hassan Nandeta, mwenyekiti wa mtaa Kinyerezi akizungumza kwa niaba ya wenyeviti wa maeneo tajwa ameishukuru DAWASA kwa ushirikishwaji katika zoezi hilo ambapo ameahidi kuwa balozi wa huduma za Maji katika mtaa wake

“Jambo hili ni lenye manufaa na tija kwani sisi kama wawakilishi wa wananchi tumepata fursa ya kuona juhudi zinazofanywa na DAWASA, hakika kwa hili mnastahili pongezi”

Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wamekuwa kiungo muhimu kati ya DAWASA na wananchi, wakirahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi na kushirikiana katika kutatua changamoto zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa mradi.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments