Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeungana na Taasis za Serikali na Binafsi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika ngazi ya Mkoa katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam.

Maadhimisho hayo yameongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Albert Chalamila, yalibeba kauli mbiu isemayo “Uchaguzi mkuu 2025 utuletee viongozi wanaojali na kuthamini haki na maslahi ya wafanyakazi, sote tushiriki.”
Katika maadhimisho hayo, DAWASA imejitokeza kwa kishindo kwa kuonesha mafanikio katika usimamizi na uboreshaji huduma za Majisafi na Usafi wa mazingira kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani.
Maadhimisho hayo yamehudhuliwa na maelfu ya Wafanyakazi kutoka Sekta na Taasisi mbalimbali yaliyotanguliwa na maandamano, burudani na hotuba kutoka viongozi wa vyama vya wafanyakazi.
