Sunday, December 21, 2025
spot_img
HomeHabariDAWASA yatekeleza agizo la Waziri Aweso Uchimbaji wa Visima

DAWASA yatekeleza agizo la Waziri Aweso Uchimbaji wa Visima

▪︎ Yakabidhi vifaa vya uchimbaji Jimbo la Kivule

Mbunge wa Jimbo la Kivule Masaburi ameshuhudia zoezi la kukabidhi vifaa vya uchimbaji wa visima katika Jimbo hilo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso aliloiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa maji kwa wananchi.

Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa vya uchimbaji katika Jimbo la Kivule, Mbunge wa Jimbo la Kivule, Masaburi amesema anaishukuru Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ahadi ya kuchimba visima ili kukidhi mahitaji ya maji kwa wananchi walio wengi.

“Mhe. Waziri Aweso aliahidi kutuletea milioni 500 za uchimbaji wa visima na sasa tunamshukuru kwa kufanikisha ahadi hiyo na sasa kazi imeanza,” amesema Mbunge.

Lakini pia tunashukuru kwa fedha alizotoa katika Jimbo letu kuboresha huduma ya maji alipofanya ziara yake hapa kwetu, utoaji wa maji kutoka tenki la Bangulo unaendelea na wananchi watapata huduma ya maji.

Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Mkama Bwire amesema kuwa kwa ujumla kazi inahusisha uchimbaji wa visima 14 ambapo kwa Jimbo la Ilala vitachimbwa visima 5 na katika Jimbo la Kivule vitachimbwa visima 9 vitakavyohudumia wananchi.

Ameongeza kuwa kwa Jimbo la Kivule, visima vitachimbwa katika maeneo ya Kivule, Magole A, Kerezange, Bombambili na Msongola mtaa wa Kidole.

“Mamlaka imepokea maelekezo yote na kazi itafanyika usiku na mchana kuhakikisha zoezi hili la visima linaenda kwa kasi na wananchi wanaanza kupata maji kikamilifu,” ameeleza Mhandisi Bwire.

Ameeleza jitihada zilizofanywa na Mamlaka ikiwemo za kufufua visima vilivyopo katika maeneo ya Mwananyamala, Tandale, Mburahati ambapo tayari visima 14 vinatoa huduma kikamilifu.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisment -
NMB Tanzania

Most Popular

Recent Comments