Dereva wa TPA na wenzake 7 washtakiwa kwa wizi wa mafuta Lita milioni 9.9

DEREVA wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ,Tino  Ndekela na wenzake saba, wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashitaka 20 liliwemo la wizi wa mafuta ya Petrol na dizel zaidi ya lota milioni 9.9 na kuisababishia hasara Kampuni ya Kimataifa ya kuhifadhi Mafuta (TIPER) Tanzania ya zaidi ya sh bilioni 26.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni  mfanyabiashara Fikiri Kidevu, Amani  Yamba, Mselem Abdallah , Kika Sanguti, Twaha Salum, Gaudence Shayo na Hamisi Hamisi, ambao walisomewa mashitaka yao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Beda Nyaki.

Washitakiwa hao walisomewa mashitaka yao  na wakili wa serikali Cathbert Mbilingi ambapo alidai walitenda makosa hayo kati ya Januari mosi mwaka 2019 hadi Desemba 31 mwaka 2022, eneo la Tungi, Kigamboni , Dar es Salaam.

Akiwasomea mashitaka hayo ilidaiwa kwamba, wanakabiliwa na mshitaka mawili ya uharibifu wa mali wanayodaiwa kutenda kati ya Januari mosi mwaka 2019 na Desemba 31 mwaka 2022 Kigamboni ambapo waliharibu bomba la kusafirishia mafuta aina ya petroli na Dizel mali ya kampuni ya Tiper.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *