Kocha wa zamani wa Simba SC, Didier Gomes Da Rosa, amefutwa kazi kama kocha mkuu wa klabu ya Al-Adalah inayoshiriki Ligi ya Daraja la Kwanza nchini Saudi Arabia, kufuatia mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha.
Klabu hiyo imethibitisha kuachana na kocha huyo raia wa Ufaransa baada ya timu kushinda michezo miwili pekee kati ya 18 aliyoiiongoza, huku ikipambana kujinusuru kushuka daraja.
Kwa sasa, Al-Adalah ipo katika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 17 baada ya kucheza mechi 15, hali inayoongeza presha ya kupambana kubaki kwenye ligi hiyo.
Gomes Da Rosa anakumbukwa zaidi kwa kazi yake ndani ya Simba SC, aliyoifundisha kuanzia Januari 2021 hadi Oktoba 2021, kabla ya kuondoka.
Mbali na Simba, kocha huyo amewahi pia kuzinoa klabu mbalimbali barani Afrika ikiwemo Al-Merreikh SC, Al Ahli Tripoli na Horoya AC, pamoja na kufundisha timu za taifa za Botswana na Mauritania.




