“Mazoezi ya awali na mbinu nyingine mbalimbali kwa kujenga uimara wa mwili kupitia mazoezi kama vile kukimbia, mazoezi ya nguvu na mazoezi mfano wa hayo. Pia, kuiandaa akili ili kuikabili michezo na mashindano kwa ujumla, wataalamu husema mafanikio huanza katika fikra,” amesema Dk. Biteko.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ametoa rai hiyo Septemba 7, 2025 katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza wakati akifungua rasmi mashindano ya 39 ya SHIMIWI yaliyotanguliwa na maandamano ya watumishi wa umma.




