Dk. Mpango aipongeza CTI tuzo za PMAYA

MAKAMU wa Rais, Dk. Philip Mpango amelipongeza Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI) kwa kuratibu vyema tuzo za wenye viwanda tangu kuanzishwa kwake.

Ametoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutoa tuzo za Rais kwa Mzalishaji Bora wa Mwaka Viwandani zinazoratibiwa na CTI), President Manufacturer of the Year Award (PMAYA).

Katika tuzo hizo Kampuni ya Sigara TCC iliibuka mshindi wa kwanza ikifuatiwa na kampuni ya bidhaa za plastiki ya Plasco Limited na Kampuni ya Mabati ya ALAF Limited.

Makamu wa Rais amesema tuzo hizo zimekuwa chachu kubwa ya maendeleo ya viwanda ambavyo vimekuwa nguzo kubwa ya ukuaji wa uchumi kutokana na kuzalisha ajira nyingi.

Amesema sekta ya viwanda ni chimbuko la maendeleo ya nchi na ina fursa kubwa ya kukua haraka na kutengeneza fursa za ajira na kuchochea bunifu na maendeleo ya teknolojia.

Alisema sekta ya viwanda ni eneo muhimu la kuongeza ajira nchini na kuliongezea taifa fedha za kigeni na inamchango kwenye ukuaji wa sekta zingine kutokana na kuzalisha bidhaa zinazouzwa nje na ndani ya nchi.

“Licha ya umuhimu mkubwa wa sekya ya viwanda kwenye ukuaji wa pato la taifa, mchango wa sekta hiyo hapa nchini bado ni mdogo sana kwa hiyo wenye viwanda wanapaswa kupambana kukuza sekta hiyo,” amesema na kuongeza kuwa;

 â€œNakumbuka mwaka 20021 niliwapa changamoto  na leo hii narudia tena kuwataka muongeze mchango wenu katika mapato ya fedha za kigeni kwenye uchumi wetu na kwenye ajira rasmi,” amesema

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *