Waziri Mkuu mteule, Dk. Mwigulu Nchemba amesema atahakikisha ndoto ya Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan ya kutengeneza ajira milioni 8 inatimia kwa kuweka utaratibu bora.
Dk Mwigulu ambaye ni Kiongozi na Msimamizi wa shughuli za Serikali bungeni ameeleza hayo leo Novemba 13, 2025 bungeni jijini Dodoma, muda mchache baada ya kuthibitishwa na Bunge, akisema watafanya uratibu na usimamizi ili kutimiza ndoto ya Dk Samia ya vijana kupata ajira.
“Tutaweka utaratibu na mpango mkakati ndani ya Serikali na kushirikisha sekta binafsi ili kuhakikisha dira ya mheshimiwa Rais (Samia) ya kutengeza ajira zisizopungua milioni 8 inakwenda kutumia,”




