“Asante mwenyekiti. Nikiwa mwenyeji nina machache ya kusema. Nianze kwa kumshukuru Mwenyezimungu kwa kutuwezesha kufika siku ya leo na kushiriki mkutano huu wa 24 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Ninawakaribisha pia Tanzania hususan hapa Arusha mkoa ambao ni Makao Makuu ya Jumuiya yetu tangu kuanzishwa kwake,”Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.