Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan amesema muhula wa pili wa awamu ya sita Serikali itatekeleza miradi, kisha baadaye wataungana na mashirika.
“Hatutakaa kusubiri, tunauza mradi, tunakwenda kubembeleza, mradi unakubaliwa, lakini nendeni mkarekebishe ili, nendeni…mara ‘objection’(pingamizi).
“Hatusubiria hayo, tutaanza kwa fedha za ndani, wao wakimaliza objection zao watatuunga Katikati. Huu si wajibu wa Rais, ni wetu sote, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, yupo pale wanatusikia, huu ndio mwendo tutakaoenda nao,” amesema.
Dkt Samia amesema aliahidi kufanya mambo ndani ya siku 100, hivyo mawaziri walioapa kama ahadi hizo zinagusa Wizara yake, waende wakazitekeleze kwa kasi.




