“Nawapongeza viongozi wa sasa na wa zamani wa taasisi. Ninayo furaha ya kwamba tunaposherehekea miaka 25 Jumuiya ya Afrika Mashariki inazidi kuimarika na kuelekea kwenye mtangamano thabiti zaidi.
Kama tunavyosema kwenye wimbo wetu wa Afrika unasema ‘Jumuiya yetu tuilinde, tuwajibike, na iimarike. Umoja wetu ndio nguvu yetu au nguzo yetu.
Idumu Jumuiya yetu’. Tumeweka maneno haya kwenye wimbo wetu ili tuwe sehemu kudumu kwa Jumuiya yetu iwe sehemu ya kufikia Afrika tunayoitaka,”Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.